Mama ee

Front Cover
East African Publishers, 1987 - Kenya - 98 pages
3 Reviews
 

What people are saying - Write a review

User Review - Flag as inappropriate

Tamthilia hii inaisawiri jamii ya kisasa ambapo wanaume waliosoma wanajificha kwenye utamaduni ili kumnyima mwanamke haki zake. Asasi ya ndoa imekumbwa na migogoro mingi na suluhu lenyewe haliwezi kupatikana kwenye kanisa, mahakama ama utamaduni bali washiriki wenyewe ndio wanaweza kuusuluhisha. Aidha mwandishi azungumzia dhuluma anayoipitia mwanamke yeyote hasa katika ndoa. Hadithi hii inaibua hisia kali kwa msomaji huku ikimpelekea kumsononekea Mwavita na Tenge walipodhulumiwa na kutukanwa kama mbwa koko na hta kutengwa kwa wanajamii. Hata hivyo kuna matumaini katika kizazi kijacho kwani mwanamke yu tayari kupambana na walimwengu kujikomboa kwa kila hali. 

User Review - Flag as inappropriate

kwa hakika tamthilia hii inafaa zaidi hasa kwa ulimwngu wa sasa ambapo wanawake wamebeswa na kuduniswa . wao wamedhihirishwa kama vyombo ombwe wasio na akili kamwe. Basi na ikiwa ipo , haina maana kwa jamii maana hawana ushauri wowote anavyotuchorea mwandishi. katika sura ya kwanza, mwanamke amesawiriwa kama chombo tu cha kumtimizia mwanamume mahitaji yake. hana uhuru wowote ule na hafai kushauriwa sababu amelipiwa mahari anavyodai Bw. Kinaya. Jambo hili kwa hakika linatuashiria mtazamo wa jamii kuhusiana na ndoa. Kwa jamii,wanawake wamechorwa kama washerati ama hawara. Shughuli yao muhimu ni kushiriki kwenye masuala ambayo hafai na wale ambao wanaonekana kuwa wasomi haki zao zinakiukwa na kulazimisha kutii amri ya wanaume. imetolewa na OBED OBURE 

Selected pages

Contents

Section 1
1
Section 2
16
Section 3
54
Copyright

Other editions - View all

Bibliographic information